Jumamosi, 26 Julai 2025

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM

Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau.

Zifuatazo ni faida za mti wa jerusalem :

1.Hutibu kisukari.

2.Hutibu Henia au ngiri.

3.Hutibu chango la kina mama.

4.Hutibu magonjwa ya zinaa.

5.Hutibu sikio linalotoa usaha.

6.Hutibu maumivu ya jino.

7.Mauwa yake hutumika kama fusho safi.

Jinsi ya kutumia mti wa jerusalemu:

1.Chukua mizizi yake na uchemshe kunywa maji yake.

2.Chukua mauwa yake na uyakaushe uchome kama fusho safi kujifukiza.

3.Fikicha majani yake na utie matone machache katika sikio linalotoa usaha.

MZUGWA

MZUGWA/MPATAKUVA

Ni dawa asili ambayo hupatikana katika sehemu tofauti za afrika mashariki na sehemu nyinginezo ambao mti wake husaoidia kama mmea wa jadi kutibu matatizo mbalimbali na kuweza kuponya na kuleta ahueni.

Zifuatazo ni faida za mzugwa/mpatakuva katika tiba asili:

1.Husaidia kuondoa mchafuko wa tumbo.

2.Husaidia kurekebisha mirija ya uzazi.

3.Hutibu malaria.

4.Hutibu uti.

5Huondoa maumivu ya hedhi na kurekebisha mfumo wa hedhi kwa wakina mama.

Jinsi ya utumia mzugwa:

1.Chukua majani yake uponde na maji kiasi kupata maji yake na kuweza kuchuja katika chupa nakutumia kama dawa nusu kikombe cha chai kutwa mara mbili kwa siku au kikombe kimoja kwa siku.

Senega/Mizizi ya Senega

Mizizi ya Senega

Mzizi wa Senega, Ni dawa ya mitishamba, uliotokea Amerika Kaskazini. Ilitumiwa sana na makabila ya asili ya Amerika, haswa watu wa Senecas katika matumizi mbalimbali kutokana na faida zake.

Faida ya mzizi wa Senega katika Tiba ya Asili:

1. Kutuliza kikohozi Hupunguza kikohozi kikavu.

2.Husaidia kuondoa sumu mwilini.

3.Huchochea mfumo wa neva na kuboresha umakini.

4.Husaidia kuondoa maumivu ya meno.

5.Husaidia kuondoa tatizo la pumu na kurahisisha upumuaji.

6.Huondoa magonjwa ya mfumo wa hewa muwako wa koo,pua,kifua na mapafu haswa katika matatizo ya pumnzi.

7.Hutibu tatizo la kambaku na kutuliza kabisa.

Jinsi ya kutumia mizizi ya senega:

1.Mzizi wa senega chemsha pamoja arkasusi unywe 1/2 kikombe kidogo cha chai mara 2 kwa wiki mbili.

Tahadhari:Inaweza kuwasha tumbo au koo kwa viwango vya juu. Epuka wakati wa ujauzito au kunyonyesha. Inaweza kusababisha kichefuchefu, kutapika, au kizunguzungu .

Ijumaa, 25 Julai 2025

Haluli

Haluli

Haluli,Ni dawa ya asili za Afrika Mashariki husaidia matatizo mbalimbali katika mwili wa binadamu kama vile kuchochea haja kubwa ili kupunguza kuvimbiwa. Hata hivyo, kusafisha tumbo au kusafisha mfumo wa usagaji chakula na mambo hutumika kusafisha tumbo na kuondokana na kuvimbiwa. Inaweza kusaidia kuondoa sumu mwilini na kuboresha usagaji chakula inapotumiwa kwa uangalifu mara kwa mara.

Faida na Matumizi ya Haluli:

1.Husaidia kumpa mtu hamu ya kula au kuboresha usagaji chakula

2.Husaidia ini na koloni kuondoa taka, na kuboresha hali ya ngozi.

3.Hufukuza minyoo katika tumbo.

4.Husaidia kusafisha damu.

6.Husafisha tumbo.

7.Huondoa kuvimbiwa na kuondoa gesi katika tumbo.

8.Huondoa gesi na uvimbe tumboni.

9.Hutumika katika tiba kwa ajili kusafisha mwili.

10.Hupunguza uzito.

11.Kuboresha hali ya ngozi.

Matumizi ya Haluli:

1.Inatumiwa katika madawa ya kufusha kwa kuchanganywa na dawa nyingine nakuweza kutibia.

NOTE:Mpaka upewe maelekezo na mtaalamu wa tiba.

2.Kuchemsha na dawa nyingine kama sanamaki, uwatu na haluli nakuweza kutumia.

Halilungi

Halilungi

Halilungi, Ni mbegu nyeusi chungu ambazo hutumika katika tiba asili.Dawa ambayo hutumiwa kwa madhumini mbalimbali ikiwa kwa kunywa na kujifukiza.

Faida za Halilungi katika tiba asili:

1. Huondoa tatizo la gesi kwenye tumbo hivyo kuondoa kuvimbiwa.

2. Hutumika kusafisha tumbo.

3. Hufukuza minyoo ya matumbo .

4. Hupunguza uzito kufanya mwili "mwepesi" na kuboresha usagaji chakula.

5. Huondoa sumu kwenye damu.

6. Husaidia kuondoa sumu kwenye ini.

7. Hutumika katika tiba kusafisha mwili kwa kutumia moshi wake au kujifusha.

8. Hufanya hamu ya kula .

Jinsi ya kutumia halilungi:

1.Kuchemsha mbegu zake na tangawizi na mdalasini na habat soda kwa dakika 10-15 na Kunywa ikipoa.1/2 kikombe kidogo cha chai.

2.Kujifukiza kwa matibabu ya kusafisha mwili.

NOTE:Mpaka upewe maelekezo na mtaalamu wa tiba.

Tahadhari:Tumia mara moja au mbili kwa wiki - sio kila siku. Inaweza kusababisha kuhara au tumbo kuuma ikiwa imezidi kipimo. Haipendekezi kwa wanawake wajawazito, watoto wadogo, au wagonjwa dhaifu bila mwongozo.

Alhamisi, 24 Julai 2025

Ginseng/Mizizi ya Ginseng

Ginseng

Ginseng,Ni mmea wa kudumu unaokua polepole ambao mizizi yake hutumiwa kama dawa katika tiba asili katika nchi mbalimbali kama China ,Korea na nchi nyenginezo.Kuna aina mbili za Ginseng ambayo ni ginseng ya Asia na ginseng ya Amerika. Ginseng pia mizizi yake hutumiwa sana katika uponyaji wa matatizo mbalimbali.

Faida za mizizi ya Ginseng katika tiba asili:

1.Husaidia kupambana na uchovu wa akili kwa wale wanaokosa usingizi.

2.Huongeza Nguvu za Kimwili kwa watu walio na uchovu sugu.

3.Husaidia mwili kupambana na maambukizi wakati wa baridi au milipuko ya magonjwa.

4.Husaidia kurekebisha shinikizo la damu na cholesterol.

5.Husaidia mwili kukabiliana na msongo wa ma wazo, kimwili au kiakili.

6.Anti-Aging Inalinda seli kutokana na uharibifu na kuifanya ngozi katika hali nzuri ya afya.

7.Husaidia katika kudhibiti kisukari mwilini.

Jinsi ya kutumia ginseng katika tiba asili:

1.Mizizi iliyokauka chemsha kwenye chai na uweze kutumia 1/2 kikombe kidogo kutwa mara mbili kwa wiki 2 .

Tahadhari:Epuka ikiwa una shinikizo la damu, una mjamzito, au unachukua vichocheo. Inaweza kusababisha kukosa usingizi au kuwashwa ikitumiwa kupita kiasi.

Shabu

Shabu

Shabu,Ni madini yenye rangi nyeupe hujulikana kwa sifa yake ya kutibia katika tiba asili ambayo ipo katika mfumo wa vipandepande,Shabu ni anti-bacterial na anti-septic yenye nguvu hutumiwa sana katika dawa za asili kutokana na sifa zake za uponyaji.

Faida shabu katika tiba asili:

1.Antiseptic na antibacterial Inazuia maambukizo ya bakteria kwenye majeraha.

2.Hutumika kusafisha maji machafu kwa kuweka kiasi kidogo .

3.Huondoa harufu mbaya ya mwilini.

4.Husaidia kutibu fangasi za miguu.

5.Hutibu vidonda vya mdomoni, harufu mbaya mdomoni na matatizo ya fizi.

6.Hukausha chunusi na kusafisha ngozi ya mafuta .

7.Huzuia kutokwa na damu kidogo kutokana na kupunguzwa kwa kunyoa au majeraha madogo.

Jinsi ya kutumia shabu katika tiba asili:

1.Jipake unga wa shabu kwapani baada ya kuoga kuondoa harufu mbaya.

2.Tia kijiwe kidogo cha shabu katika maji ya moto na suuza kinywa (usimeze).

3.Paka unga wa shabu kwenye majeraha madogo kusasidia kukata damu

4.Changanya poda ya shabu na maji ya moto, loweka miguu au weka kibandiko kwenye eneo lililoathirika na fangasi.

5.Paka maji ya shabu kwenye chunusi kwa kutumia pamba;kwa dakika 15 halafu safisha.

6.Baada ya kunyoa Sugua na shabu kwenye ngozi ili kuziba vinyweleo na kuacha kuvuja damu.

Tahadhari:Unapotumia shabu Usitumie kwa kiasi kikubwa na Usitumie kwenye majeraha ya yalochimbika au maeneo nyeti mfano macho na sehemu za siri. Tumia kwa wastani ili kuzuia kuwashwa au kukauka sana kwa ngozi.

Beetroot

Beetroot

Beetroot,Ni mboga ambazo huota viazi vyenye rangi nyekundu au zambarau vinavyotumika katika matumizi mbalimbali. Ni mboga yenye virutubishi vingi iliyojaa vitamini na madini. Beetroot ni kiungo kinachotumiwa sana katika maandalizi mbalimbali ya upishi, kutoka kwa saladi na supu hadi juisi na vyakula mbalimbali.

Faida za beetroot:

1.Husaidia kuondoa sumu mwilini.

2.Husaidia afya ya ini na usagaji chakula.

3.Kupunguza uvimbe mwili.

4.Husaidia kudhibiti uzito mwilini.

5.Kuimarisha afya ya ngozi kwa kukuza ngozi yenye afya.

Jinsi ya kutumia beetroot:

1.Beetroot 1 saga na kufanya juisi unaweza pia kuchanganya na matunda.Kunywa 1/4 hadi 1/2 kikombe cha juisi safi ya beetroot mara moja au mbili kwa siku.

2.Beetroot unaweza kukata na kuchanganya na mbogamboga nyingine kama salad na kuweza kutumia kama mlo.

Jumatano, 23 Julai 2025

KIWI/MKIWI

MKIWI

Mti wa kiwi,unajulikana zaidi kwa matunda yake,lakini pia sehemu nyingine za mmea wake kama majani, mizizi, na magome hutumika katika tiba asili kama dawa inayotibu.Mmea huu haswa hutumiwa katika nchi za Kichina na Kikorea.

Faida za mmea wa kiwi

1. Tunda:
i.Husaidia mfumo wa umeng'enyaji.
ii.Hupunguza shinikizo la damu na cholesterol.
iii.Huisaidia ngozi ufanya kuondokana na makunyanzi.
iv.Husaidia kuondoa gesi tumboni.

2. Majani Faida za kiafya:
i.Husaidia kupunguza uvimbe katika mwili.
ii.Hutumika kutibu majeraha katika mwili.
iii.Inatumika katika kutibu kikohozi .

3. Mizizi Faida za kiafya:
i.Husaidia kusafisha ini na damu.
ii.Hutibu homa ya manjano na homa ya ini.
iii.Husaidia kusafisha figo.

4.Gome:
i.Husaidia kukaza ngozi na kupunguza uvimbe na muwasho.

Jinsi ya kutumia.

1.Matunda: Husagwa juisi.

2.Majani: Majani yaliyokaushwa au mabichi yaliyokaushwa kwenye maji ya moto (dakika 10-15). Kunywa mara 1-2 kwa siku.

3.Mizizi: Chemsha 5-10g ya mizizi iliyokauka katika vikombe 2 vya maji, chemsha kwa dakika 15-20, na kunywa kikombe nusu kila siku. Poda ya majani mabichi na upake kwenye majeraha au ngozi iliyovimba.

Ijumaa, 2 Mei 2025

MTOMOKWA/MTOPETOPE

MTOMOKWA/MTOPETOPE

Mtomokwa/Mtopetope pori,Ni mmea unaozaa matunda yanayoitwa matomokwa ambayo yanakuwa na muonekano wa kijani au wekundu kwa nje ndani ikiwa na nyama nyeupe zenye kokwa nyeusi unaotumiwa sana katika dawa za asili za Kiafrika. Inakua katika sehemu nyingi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na inathaminiwa sana kwa umuhimu wake wa matibabu. Sehemu zinazotumika katika dawa asili ni Majani Gome (shina na gome la mizizi).

Faida za mtomokwa katika tiba asili:

1. Majani hutibu maambukizi ya ngozi uvimbe na maumivu ya viungo na majeraha.

2.Majani yake husaidia kupunguza homa (pamoja na inayohusiana na malaria).

3.Majani yake hutumika kwa kikohozi, pumu, na maumivu ya kifua.

4.Majani yake huondoa maumivu ya tumbo na kuhara.

5.Magome yake hutibu maambukizi ya bakteria na magonjwa ya zinaa.

6.Magome yake hutumika kwa maumivu ya meno na mwili.

7.Magome yake husaidia kuondoa sumu kupitia mkojo.

8. Mizizi hutumika kwa minyoo ya matumbo.

Jinsi ya kutumia:

1.Chemsha:Majani mabichi au yaliyokaushwa (kiganja) kwenye maji ya moto kwa dakika 10-15. Kunywa kikombe 1, mara 2-3 kwa siku.

2.Bandika:Majani mabichi yaliyosagwa bandika moja kwa moja kwenye majeraha au maeneo yaliyovimba.

3.Kuvuta pumzi ya mvuke: Chemsha majani na vuta mvuke kwa tatizo la kupumua.

4.Chemsha magome (10-20g) katika maji kwa dakika 15-20. Chuja na chukua kikombe nusu mara 2 kwa siku.

5.Dawa ya maumivu ya jino: Tafuna kipande kidogo cha gome la shina au maji ulorowekea magome yake kuosha kinywa au kuskutuwa.

6.Chemsha vipande vidogo vya mizizi iliyokatwa (5-10g) katika maji, chuja, na unywe kwa kiasi (1/4-1/2 kikombe, mara moja au mbili kwa siku).

MLANGAMIA

MLANGAMIA

Mlangamia,Ni mti ambao shina lipo chini mti upo juu huwa na sifa mfano wa kambakamba au nywelenywele unapoota hauonyeshi kuwa unaelekea wapi ambao hutumika katika tamaduni mbalimbali.

Faida za Mlangamia katika tiba asilli:

1.Husaidia kupunguza uvimbe na kukuza uponyaji wa majeraha.

2.Husaidia tatizo la kwikwi yenye muendelezo.

3.Husaidia ngozi ya kichwa na kukuza ukuaji wa nywele.Inatumika kuimarisha nywele, kupunguza mba, na kuchochea ukuaji.

4.Husaidia kuondoa maumivu ya tumbo la hedhi/chango la wakina mama.

5.Husaidia kuondoa homa za msimu kwa kuchanganywa na miti mingine katika kujifukiza.

6.Husaidia kusafisha mfumo wa uzazi .

7.Huondoa maumivu ya tumbo kwa watoto na watu wazima pia.

8.Hutumiwa kusafisha ngozi.

9.Husaidia mtoto aliebemendwa kwa kunyweshwa na kuogea.

10.Huondoa homa za upepo na kuupa mwili nguvu kwa kujifukiza nyungungu.

Jinsi ya kutumia mlangamia katika tiba asili:

1.Kwa majeraha au kuvimba:kuchemshwa kwa maji na yakipoa osha moja kwa moja kwenye ngozi.Nakamba zake twanga na ubandike kwenye kidonda

2.Kwa kusafisha mirija ya uzazi:Chemsha mlangamia kwa maji na kunywa 1/4(Robo) kikombe cha chai.

3. Matibabu ya Nywele chemsha na kutumia kusuuza katika ngozi ya kichwa.

4.Kwa kwikwi:Chukua kamba za mlangamia na chembe za ubani 3.

5.Kwa mtoto aliebemendwa anyweshwe na kuogeshwa.Maji ya kuogeshwa wapekeche kamba hizo kwenye chombo wazazi wake na kumuogeshea mtoto huyo siku 21.

6.Kwa tumbo kamba zake ponda na maji uchuje unywe urojo wake kwa robo kikombe kutwa mara 2.

Zingatio:Hizo ni faida za mlangamia kwa uchache kuna faida nyingi zinapatika katika kamba zake na kiazi chake kwa ujumla kutokana na matumizi mbalimbali katika jamii tofauti.

MLANGILANGI

MLANGILANGI

Mlangilangi, Ni mti wa kitropiki uliotokea Kusini-mashariki mwa Asia na sehemu nyingine za dunia na kwa uchache Afrika Mashariki. Ni maarufu zaidi kwa maua yake yenye harufu nzuri yaitwayo malangilangi.

Faida za mlangilangi katika Tiba ya Asili

1.Kutuliza na kupunguza mafadhaiko, wasiwasi, na unyogovu. .

2.Majeraha madogo, michubuko na maambukizo ya ngozi.

3.Utunzaji wa nywele kwa mafuta yake.

4.Husaidia ngozi kwa kuondoa chunusi na mba.

5.Hutumiwa kupunguza shinikizo la damu na mapigo ya moyo tulivu.

6.Husaidia kulainisha nywele na ngozi ya kichwa.

Jinsi ya kutumia mlangilangi:

1. Maua (Safi au Kavu)

A:Kunywa:
Kipimo:Maua safi (1-2 gramu) au Maua yaliyokaushwa kijiko 1 ( 0.5-1 gramu)
Tumia:Mimina katika kikombe 1 cha maji ya moto kwa dakika 10 Kunywa mara 1-2 kila siku kwa kutuliza, kupunguza mkazo, au msaada wa kulala.

B.Kuogea:Maua safi au vijiko 1-2 vya maua kavu tia katika maji ya moto,roweka kwa dakika 20-30.

C.Kupaka:Ponda maua 2-3 na uitumie kwa eneo lililoathirika. Acha kwa dakika 15-20 mara moja kwa siku.

2.Majani
A.Majani safi 5-7 au kijiko 1 cha majani makavu kwa vikombe 2 vya maji.

Tumia: Chemsha kwa dakika 10-15, shida. Inaweza kutumika kama kuosha mwili au kunywewa kama chai kali (½ kikombe mara 1-2 kwa siku). Tumia kwa siku 3-5 pekee kwa wakati mmoja kwa matumizi ya ndani.

B.Ponda:
Kipimo:Ponda majani 3-5 safi
Tumia:funika na kitambaa. Tumia hadi mara 2 kwa siku.

3.Gome
A.Chemsha:
Kipimo: Vipande 1-2 vidogo vya gome (takriban 1-2 gramu) kwa vikombe 2 vya maji.

Tumia: Chemsha kwa dakika 15-20, baridi na shida.
Matumizi ya ndani tu chini ya uangalizi - si zaidi ya kikombe ¼ kwa siku kwa muda mfupi.

4.Mafuta
A.Masaji mauwa ya mlangilangi na mafuta mengine kama ya nazi changanya na kupaka.

B.Kuoga: Ongeza matone machache ya mafuta kwenye maji ya joto.Husaidia utulivu na kuboresha hisia.

C.Kupaka:Ongeza matone 1-2 kwa shampoo au kiyoyozi. Husaidia kulainisha nywele na ngozi ya kichwa.

Tahadhari:Usitumie gome ndani kwa muda mrefu au kwa kiasi kikubwa, pia wajawazito na wanaonyonyesha wasitumie isipokua mafuta yake.

Alhamisi, 1 Mei 2025

MKUNDE NYIKA/MKUNDE PORI/MNUKA UVUNDO

MKUNDE NYIKA/MKUNDE PORI/MNUKA UVUNDO

Mkunde Nyika ni mti wa asili unaopatikana katika baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki, hasa katika nchi kama Tanzania na Kenya. Mti huu unajulikana kwa matumizi yake katika tiba za asili, ambapo sehemu mbalimbali za mti, kama vile majani na mizizi, hutumika kutengeneza dawa za kutibu magonjwa mbalimbali.

Faida za mkunde nyika katika tiba asili:

1.Hutibu magonjwa kama vile homa, maumivu ya tumbo, na matatizo ya ngozi.

2.Hutumika kutibu maumivu ya kifua .

3.Husafisha mfumo wa mkojo na kuondoa muwasho wa sehemu za siri.

4.Husaidia kutibu matatizo ya tumbo kama tumbo la uzazi, hedhi na mchafuko wa tumbo.

5.Hutibu u.t.i na fangasi sugu sehemu nyeti.

6.Husaidia kukausha vidonda na kuondoa mapele muwasho katika ngozi.

7.Husaidia kuzibua mirija iliyoziba katika mfumo wa uzazi.

Jinsi ya kutumia mkunde pori/mkunde nyika:

1.Chemsha mizizi yake na uweze kutumia nusu kikombe kwa siku mara mbili kwa mwezi.

2.Majani yake ponda na uweze kubandika katika sehemu ya ngozi ambayo imeathirika.

Tahadhari:Angalizo kwa wamama wajawazito tayari wastumie dawa hii inaweza kuleta athari ndani ya kipindi hicho.

MKILUA

MKILUA

Mkilua,Ni mmea adimu ambao hutoa maua hujulikana kwa jina la vilua.Mara nyingi inapatikana katika mikoa ya mwambao wa Afrika Mashariki, hasa nchini Tanzania na Kenya.

Faida za mkilua katika tiba asili:

1.Husaidia kutibu matatizo ya kupumua.

2.Husaidia ngozi kwa ajili ya majeraha na uvimbe .

3.Husaidia usagaji chakula.

Jinsi ya Kutumia Mkilua katika tiba asili:

1.Chai:Majani kutibu magonjwa madogo kama vile kikohozi au matatizo ya usagaji chakula.

2.Majani:Majani yaliyosagwa hutumika kwenye ngozi kwa ajili ya majeraha, maambukizi au uvimbe.

3.Mafuta:Mafuta ya asili kama ya nazi yanaweza kuchanganywa na mauwa ya mkilua na kuleta harufu nzuri ya kuburudisha au kama manukato.

Mzio:Wakati mwingine kutokana na harufu kali sana ya mauwa ya mkilua yanaweza kusababisha mzio .

KIVUMBASI/KIVUMBASHA

KIVUMBASI

Kivumbasi ni mmea wa dawa unaotumika sana katika tiba za asili nchini Tanzania na maeneo mengine ya Afrika Mashariki. Ingawa kuna mimea kadhaa inayojulikana kwa jina hili kulingana na eneo na kabila, moja ya mimea inayojulikana zaidi kama Kivumbasi ni aina ya mimea yenye harufu nzuri(ambayo ni pamoja na mimea ya mnanaa na majani ya chai).

Faida za Kivumbasi katika tiba asili:

1.Kivumbasi hutibu uzazi ulifungwa kiuchawi.

2.Hutibu tatio la kikohozi na mafua.

3.Kivumbasi hutuliza maumivu ya kichwa na mwili.

4.Kivumbasi na manyoya ya kuku na mbuzi ukimfusha mtu mwenye degedege anapona.

5.Kivumbasi ukinywa kwa wingi hutoa uchawi mwilini.

6.Maji ya kivumbasi huondoa uchovu na kuongeza nguvu.

7.Kivumbasi hutibu na tatizo la presha.

8.Husafisha nyumba na mambo ya kisihiri.

9.kivumbasi huondoa nuksi mwilini jifukize Na kunywa kwa siku 14.

10.Hutoa mafuta mwilini kwa kupunguza unene.

11.Hutibu magonjwa ya tumbo na kwa wasioona siku zao/hedhi.

12.Husaidia kwa mtoto mchanga asiyepata choo.

13.Kivumbasi kwa aliyekumbwa Na jini mbaya na athari zote alizosababishiwa na jini.

Jinsi ya kutumia kivumbasi katika tiba asili:

1.Anayeumwa tumbo anywe kwa nusu kikombe kwa mtu mzima na mtoto basi mpe kijiko kimoja cha maji ya kivumbasi.

2.Dekia maji ya majani ya kivumbasi pia choma kivumbasi kikavu ufukize moshi wake.

3.Maji ya kivumbasi kwa wingi nakuoga athari zilizompata kwa upepo mbaya zitaondoka.

4.Majani yake huchemshwa na mvuke wake kujifukiza .

5.Kivumbasi kikavu na unga wa sembe kichome pamoja kwa kusafisha nyumba.

6.Chemsha kivumbasi Na kunde mbichi Saba hutoa kifungo cha mwanamke aliyefanyiwa sihiri asipate mimba.

7.Manyoya ya mbuzi na ya kuku basi unamfukiza mtu aliyeanguka mtu mwenye degedege atapona.

Jumapili, 27 Aprili 2025

MTUNDA DAMU

MTUNDA DAMU

Mtunda Damu,Ni mti unaozaa matunda ambayo hujulikani kama matunda damu, matunda hayo hujulikana kwa umbile lake dogo la dura kama zabibu na yakiwa na rangi nyekundu ambayo sehemu mbalimbali za dunia ikiwa pamoja na Afrika Mashariki.Unathaminiwa katika dawa za asili.Sehemu mbalimbali za mmea majani,magome, maua ya mtunda damu hujulikana kwa sifa zake katika kutibu maradhi mbalimbali.

Faida za Mtunda Damu katika tiba asili:

1. Husaidia mfumo wa umeng'enyaji kwa kuondoa kuvimbiwa kaatika tumbo.

2.Husaidia kuondoa tatizo la yabisi wa tumbo ambao hupelekea tatizo kupata choo kigumu.

3.Kuondoa sumu mwilini

4.Kuvimba kwa utulivu wa akili na kuboresha usingizi, na akili

5.Kukuza afya ya ngozi kutuliza ngozi kuwasha, vipele na uvimbe.Antimicrobial: Majani yaliyopondwa wakati mwingine hutumiwa kwenye majeraha.

6.Kutuliza mishipa na kuweza kuleta utulivu wa mwili.

Jinsi ya kutumia mtunda damu.

1. Majani: Anti-inflammatory: Hutumika kutuliza ngozi kuwasha, vipele na uvimbe.Antimicrobial: Majani yaliyopondwa wakati mwingine hutumiwa kwenye majeraha ili kuzuia maambukizi.Chai ya majani inaweza kusaidia kuondoa tatizo la yabisi wa tumbo.
Kipimo: Kijiko 1 cha majani makavu kwa kikombe cha maji ya moto Tumia: Mwinuko wa dakika 5-10 Kunywa mara moja kwa siku.
Matumizi:Paka chai iliyopozwa kwenye ngozi kwa kitambaa au osha au suuza katika ngozi.
Majani safi: Kusagwa na kutumika kwa maeneo yenye kuvimba kwa dakika 10-15.

2. Magome:Kutuliza na kuzuia kuhara htumiwa kwa kiasi kidogo kwa kuhara,kupunguza uvimbe na muwako wa ngozi.kusafisha jeraha au kuvuta koo kwa vidonda.
Kipimo: 1-2 gramu ya gome kavu kwa kikombe cha maji.
Tumia: Chemsha kwa dakika 10-15. Chukua mara 1-2 kwa siku ikiwa ni lazima. Kumbuka: Tumia kwa muda mfupi tu.

3. Maua:Hutumika kutuliza wasiwasi, kuboresha usingizi, na akili. Tonic ya mmeng'enyo: Husaidia na hamu duni na usagaji chakula kwa uvivu. Kupamba ngozi.
Kipimo:Kijiko 1 cha mauwa makavu kwa kikombe cha maji ya moto.
Tumia:kunywa kikombe kimoja mara 1-2 kwa siku kwa wiki.

MFYOKSI

MFYOKSI

Mfyoksi,Ni mti unaozaa matunda ambayo hujulikani kama mafyoksi pia unathaminiwa katika dawa za asili.Sehemu mbalimbali za mmea majani,magome, maua ya mfyoksi hujulikana kwa sifa zake katika kutibu maradhi mbalimbali.

Faida za Mfyoksi katika tiba asili:

1.Hutibu kutuliza ngozi yenye mwako,kuumwa na wadudu, upele

2.Huondoa hali ya kuvimbiwa kwa kusaidia mfumo wa usagaji chakula.

3.Huondoa kikohozi.

4.Kuzuia uvimbe na kupunguza kuwashwa katika ngozi.

5.Kuondoa sumu mwilini.

6.Husaidia kupunguza homa.

7.Husaidia kuondoa kichefuchefu.

Matumizi ya mfyoksi katika tiba asili:

1.kwa ngozi iliyowaka, kuumwa na wadudu, upele, kupunguza homa,kuondos kichefuchefu.
Kipimo:Kijiko 1 cha majani makavu au 1 changanya na kikombe cha maji ya moto kwa dakika 10-15.
Tumia: Kunywa kikombe 1-2 kwa siku kwa usaidizi wa usagaji chakula au kichefuchefu Poultice (kwa ngozi): Majani safi yaliyosagwa yanayotumika kwa kuumwa na wadudu au upele kwa dakika 10-15.

2.Hutuliza mfumo wa neva na inaweza kupunguza kuwashwa au wasiwasi ,hutumika kwa kikohozi kikavu au muwasho wa koo,husaidia kupunguza homa na uvimbe Kipimo: 1-2 gramu ya gome kavu kwa kikombe cha maji Kupika: dakika 15-20.
Tumia: kikombe 1 kwa siku, katika kipimo kilichogawanywa.

3.Husaidia na kuvimbiwa kidogo na usagaji chakula,hutuliza akili na kusaidia usingizi wa utulivu na Kusafisha ngozi.
Kipimo:Kijiko 1 cha maua makavu na kikombe cha maji ya moto kwa dakika 5-10.
Tumia: vikombe 1-2 kila siku ndani ya wiki.

KIBIRITI UPELE

KIBIRITI UPELE

Kibiriti Upele ,Ni madini asilia yenye historia ndefu ya kutumika katika dawa za asili ambayo ipo kwa mfumo wa poda na rangi yake ya njano.Ambayo hutumika kwa matatizo mbalimbali.

Faida za kibiriti upele katika tiba asili:

1.Husaidia kusafisha ngozi na matatizo yote ya ngozi kwa ujumla kama chunusi, ukurutu, kipele, psoriasis, magonjwa ya fangasi na mba.

2.Husaidia ini kwa kuondoa sumu mwilini.

3.maambukizi ya vimelea kutoka na sifa yake ya antibacterial, antifungal, antiparasitic, na keratolytic (peeling) .

4.Husaidia kusafisha damu mwilini.

5.Katika tiba asili hutumika pia kuondoa vitu vibaya vya kisihiri kwa kuichoma katika moto.
Note:Mpaka upewe maelekezo na mtoa huduma ya dawa asili.

6.Hutibu tatizo la minyoo tumboni.

7.Husafisha mazingira kwa kuuwa wadudu katika eneo kwa kuchoma na kuimwaga.

Matumizi ya kibiriti upele:

1.Kwa matumizi ya Ngozi iloathirika kwa m'ba,upele,mwasho, ukurutu ,fangasi ,mapunye n.k.
Kipimo:Kijiko kiasi cha 1/8 ya unga wa kibiriti upele na kiasi kichache cha maji au mafuta ya mwarobaini/Nazi.
Kutumia: Moja kwa moja kwa ngozi iliyoathiriwa, wacha ikae kwa dakika 10-20, kisha uoshe. Tumia: Mara moja kwa siku.

2.Kuondoa Sumu na Usaidizi wa Ini.
Kipimo: 125-250 mg ( 1/16 hadi 1/8 kijiko) changanya Asali, samli, au maziwa, baada ya chakula.

3.Hutumika kutibu minyoo ya matumbo.

Tahadhari:Matumizi ya nje kwa ujumla ni salama, lakini yanaweza kusababisha athari endapo itakuletea matokeo kama ukavu wa ngozi na kuwashwa unaweza ukaacha kutumia vinginevyo ni nzuri na inasaidia.

SUMAC/MCHENGELE

SUMAC/MCHENGELE

Mmea wa sumac/Mchengele,Ni kiungo kilichokaushwa kutoka katika matundaya rangi nyekundu yaliyokaushwa na kusagwa na kuweza kupatikana kwa unga ambao huitwa sumac/Mchengele.Ni kiungo ambacho hutumiwa katika nchi za Amerika, Ulaya, na Mashariki ya Kati,Ni kiungo chenye rangi nyekundu na kinachotumiwa katika vyakula kwa ladha yake tamu kama ya machumgwa au ndimu kinachotumiwa kwa sana katika nchi hizo kwa manufaa mbalimbalia ukiachia harufu yake.

Faida za mmea wa sumac katika tiba asili

1.Hupunguza uvimbe katika mwili.

2.Husaidia katika kuacha kuhara au kutibu majeraha.

3.Husaidia kuosha koo kwa matatizo ya vidonda na matatizo ya fizi.

4.Husaidia kuondoa maumivu ya misli.

5.Huondoa gesi tumboni kwa kusaidia mfumo wa umeng'enyaji chakula.

Matumizi ya sumac katika matumizi kama tiba asili:

i.Usagaji chakula au kupunguza uvimbe,kwa msaada wa kinga,Kutibu kuhara au kama kiosha kinywa kwa vidonda vya koo na matatizo ya fizi, kusaidia katika kupunguza hali kama vile maumivu ya misuli.
Kipimo: Chai (Infusion): Kipimo: vijiko 1-2 vya majani yaliyokaushwa kwa kikombe cha maji ya moto kwa dakiaka 10 hadi 15.
Tumia: Kunywa mara moja au mbili kila siku.

ii.Kusafisha majeraha.
kwa ngozi:kupakwa moja kwa moja kwenye michubuko, majeraha au ngozi iliyowashwa kwa hadi dakika 15 au 20.

Ijumaa, 25 Aprili 2025

LOZI/ALMOND

LOZI/ALMOND

Mmea wa mlozi, unaojulikana sana kwa mbegu zake zinazoitwa lozi. Lozi zinazotumika kwa manufaa mbalimbali za kiafya katika tiba asili. Sehemu za mmea wa lozi zinazotumika katika dawa za asili ikiwa ni mbegu za lozi, Mafuta ya lozi, maua ya lozi na maganda ya lozi.

Faida za lozi katika tiba asili:

1.Husaidia afya ya moyo na mishipa kwa kupunguza viwango vya cholesterol mbaya.

2.Huboresha usagaji chakula na kuzuia kuvimbiwa.

3.Huongeza ufahamu kwa kuboresha ubongo.

4.Hulainisha , kuboresha na kupunguza dalili za mikunjo katika ngozi.

Matumizi ya Lozi/Almomd katika tiba asili:

1.Mafuta ya lozi, Kipimo:Weka matone machache kwenye ngozi au nywele.
Kwa ngozi:Sugua ngozi kwa upole ili kutibu ukavu au muwasho.
Kwa nywele:Paka ndani ya kichwa na kuondoka kwa dakika 30 kabla ya kuosha.
kwa usagaji chakula au kuvimbiwa: Kijiko 1 cha mafuta ya lozi kuchanganya katika maji ya moto ili kusaidia usagaji chakula.

2.Lozi ,Hutumika kusaga na maziwa na kunywa kwa kuboresha afya ya ubongo.
Kipimo:kipimo kikombe kidogo cha kahawa na glasi moja ya maziwa mara mbili kwa siku

3. Maua ya lozi : Maua ya mlozi hutumiwa katika dawa za jadi ili kupunguza mkazo na wasiwasi, kukuza utulivu. kutibu hali ya upumuaji kama vile kikohozi.
Kipimo: Chai (Infusion): Kipimo: Vijiko 1-2 vya maua ya mlozi kavu kwa kikombe cha maji ya moto dakika 5-10 .
Tumia: Kunywa mara moja au mbili kwa siku ili kutuliza neva au kupunguza usumbufu wa kupumua.

4. Magome ya lozi: Kutuliza nafsi: Magome ya mlozi, haswa yakichemshwa, hutumiwa kwa sifa zao za kutuliza ili kusaidia kutibu kuhara.
Kipimo: Vijiko 1-2 vya maji ya magome ya mlozi yaliyochemshwa kwa dakika 15-20 .
Tumia: Kunywa kikombe 1 kwa siku, au inavyohitajika, kwa masuala ya usagaji chakula kama vile kuhara.

Tahadhari:Mzio: Watu wengine wanaweza kuwa na mzio na lozi, kwa hivyo tahadhari inashauriwa kuacha endepo inapokuletea athari mtumiaji.

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS