Alhamisi, 24 Julai 2025

Ginseng/Mizizi ya Ginseng

Ginseng

Ginseng,Ni mmea wa kudumu unaokua polepole ambao mizizi yake hutumiwa kama dawa katika tiba asili katika nchi mbalimbali kama China ,Korea na nchi nyenginezo.Kuna aina mbili za Ginseng ambayo ni ginseng ya Asia na ginseng ya Amerika. Ginseng pia mizizi yake hutumiwa sana katika uponyaji wa matatizo mbalimbali.

Faida za mizizi ya Ginseng katika tiba asili:

1.Husaidia kupambana na uchovu wa akili kwa wale wanaokosa usingizi.

2.Huongeza Nguvu za Kimwili kwa watu walio na uchovu sugu.

3.Husaidia mwili kupambana na maambukizi wakati wa baridi au milipuko ya magonjwa.

4.Husaidia kurekebisha shinikizo la damu na cholesterol.

5.Husaidia mwili kukabiliana na msongo wa ma wazo, kimwili au kiakili.

6.Anti-Aging Inalinda seli kutokana na uharibifu na kuifanya ngozi katika hali nzuri ya afya.

7.Husaidia katika kudhibiti kisukari mwilini.

Jinsi ya kutumia ginseng katika tiba asili:

1.Mizizi iliyokauka chemsha kwenye chai na uweze kutumia 1/2 kikombe kidogo kutwa mara mbili kwa wiki 2 .

Tahadhari:Epuka ikiwa una shinikizo la damu, una mjamzito, au unachukua vichocheo. Inaweza kusababisha kukosa usingizi au kuwashwa ikitumiwa kupita kiasi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS