MKIWI
Mti wa kiwi,unajulikana zaidi kwa matunda yake,lakini pia sehemu nyingine za mmea wake kama majani, mizizi, na magome hutumika katika tiba asili kama dawa inayotibu.Mmea huu haswa hutumiwa katika nchi za Kichina na Kikorea.
Faida za mmea wa kiwi
1. Tunda: i.Husaidia mfumo wa umeng'enyaji. ii.Hupunguza shinikizo la damu na cholesterol. iii.Huisaidia ngozi ufanya kuondokana na makunyanzi. iv.Husaidia kuondoa gesi tumboni.
2. Majani Faida za kiafya: i.Husaidia kupunguza uvimbe katika mwili. ii.Hutumika kutibu majeraha katika mwili. iii.Inatumika katika kutibu kikohozi .
3. Mizizi Faida za kiafya:
i.Husaidia kusafisha ini na damu.
ii.Hutibu homa ya manjano na homa ya ini.
iii.Husaidia kusafisha figo.
4.Gome: i.Husaidia kukaza ngozi na kupunguza uvimbe na muwasho.
Jinsi ya kutumia.
1.Matunda: Husagwa juisi.
2.Majani: Majani yaliyokaushwa au mabichi yaliyokaushwa kwenye maji ya moto (dakika 10-15). Kunywa mara 1-2 kwa siku.
3.Mizizi: Chemsha 5-10g ya mizizi iliyokauka katika vikombe 2 vya maji, chemsha kwa dakika 15-20, na kunywa kikombe nusu kila siku. Poda ya majani mabichi na upake kwenye majeraha au ngozi iliyovimba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni