Ijumaa, 25 Julai 2025

Halilungi

Halilungi

Halilungi, Ni mbegu nyeusi chungu ambazo hutumika katika tiba asili.Dawa ambayo hutumiwa kwa madhumini mbalimbali ikiwa kwa kunywa na kujifukiza.

Faida za Halilungi katika tiba asili:

1. Huondoa tatizo la gesi kwenye tumbo hivyo kuondoa kuvimbiwa.

2. Hutumika kusafisha tumbo.

3. Hufukuza minyoo ya matumbo .

4. Hupunguza uzito kufanya mwili "mwepesi" na kuboresha usagaji chakula.

5. Huondoa sumu kwenye damu.

6. Husaidia kuondoa sumu kwenye ini.

7. Hutumika katika tiba kusafisha mwili kwa kutumia moshi wake au kujifusha.

8. Hufanya hamu ya kula .

Jinsi ya kutumia halilungi:

1.Kuchemsha mbegu zake na tangawizi na mdalasini na habat soda kwa dakika 10-15 na Kunywa ikipoa.1/2 kikombe kidogo cha chai.

2.Kujifukiza kwa matibabu ya kusafisha mwili.

NOTE:Mpaka upewe maelekezo na mtaalamu wa tiba.

Tahadhari:Tumia mara moja au mbili kwa wiki - sio kila siku. Inaweza kusababisha kuhara au tumbo kuuma ikiwa imezidi kipimo. Haipendekezi kwa wanawake wajawazito, watoto wadogo, au wagonjwa dhaifu bila mwongozo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS