Jumapili, 27 Aprili 2025

KIBIRITI UPELE

KIBIRITI UPELE

Kibiriti Upele ,Ni madini asilia yenye historia ndefu ya kutumika katika dawa za asili ambayo ipo kwa mfumo wa poda na rangi yake ya njano.Ambayo hutumika kwa matatizo mbalimbali.

Faida za kibiriti upele katika tiba asili:

1.Husaidia kusafisha ngozi na matatizo yote ya ngozi kwa ujumla kama chunusi, ukurutu, kipele, psoriasis, magonjwa ya fangasi na mba.

2.Husaidia ini kwa kuondoa sumu mwilini.

3.maambukizi ya vimelea kutoka na sifa yake ya antibacterial, antifungal, antiparasitic, na keratolytic (peeling) .

4.Husaidia kusafisha damu mwilini.

5.Katika tiba asili hutumika pia kuondoa vitu vibaya vya kisihiri kwa kuichoma katika moto.
Note:Mpaka upewe maelekezo na mtoa huduma ya dawa asili.

6.Hutibu tatizo la minyoo tumboni.

7.Husafisha mazingira kwa kuuwa wadudu katika eneo kwa kuchoma na kuimwaga.

Matumizi ya kibiriti upele:

1.Kwa matumizi ya Ngozi iloathirika kwa m'ba,upele,mwasho, ukurutu ,fangasi ,mapunye n.k.
Kipimo:Kijiko kiasi cha 1/8 ya unga wa kibiriti upele na kiasi kichache cha maji au mafuta ya mwarobaini/Nazi.
Kutumia: Moja kwa moja kwa ngozi iliyoathiriwa, wacha ikae kwa dakika 10-20, kisha uoshe. Tumia: Mara moja kwa siku.

2.Kuondoa Sumu na Usaidizi wa Ini.
Kipimo: 125-250 mg ( 1/16 hadi 1/8 kijiko) changanya Asali, samli, au maziwa, baada ya chakula.

3.Hutumika kutibu minyoo ya matumbo.

Tahadhari:Matumizi ya nje kwa ujumla ni salama, lakini yanaweza kusababisha athari endapo itakuletea matokeo kama ukavu wa ngozi na kuwashwa unaweza ukaacha kutumia vinginevyo ni nzuri na inasaidia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS