Alhamisi, 24 Julai 2025

Shabu

Shabu

Shabu,Ni madini yenye rangi nyeupe hujulikana kwa sifa yake ya kutibia katika tiba asili ambayo ipo katika mfumo wa vipandepande,Shabu ni anti-bacterial na anti-septic yenye nguvu hutumiwa sana katika dawa za asili kutokana na sifa zake za uponyaji.

Faida shabu katika tiba asili:

1.Antiseptic na antibacterial Inazuia maambukizo ya bakteria kwenye majeraha.

2.Hutumika kusafisha maji machafu kwa kuweka kiasi kidogo .

3.Huondoa harufu mbaya ya mwilini.

4.Husaidia kutibu fangasi za miguu.

5.Hutibu vidonda vya mdomoni, harufu mbaya mdomoni na matatizo ya fizi.

6.Hukausha chunusi na kusafisha ngozi ya mafuta .

7.Huzuia kutokwa na damu kidogo kutokana na kupunguzwa kwa kunyoa au majeraha madogo.

Jinsi ya kutumia shabu katika tiba asili:

1.Jipake unga wa shabu kwapani baada ya kuoga kuondoa harufu mbaya.

2.Tia kijiwe kidogo cha shabu katika maji ya moto na suuza kinywa (usimeze).

3.Paka unga wa shabu kwenye majeraha madogo kusasidia kukata damu

4.Changanya poda ya shabu na maji ya moto, loweka miguu au weka kibandiko kwenye eneo lililoathirika na fangasi.

5.Paka maji ya shabu kwenye chunusi kwa kutumia pamba;kwa dakika 15 halafu safisha.

6.Baada ya kunyoa Sugua na shabu kwenye ngozi ili kuziba vinyweleo na kuacha kuvuja damu.

Tahadhari:Unapotumia shabu Usitumie kwa kiasi kikubwa na Usitumie kwenye majeraha ya yalochimbika au maeneo nyeti mfano macho na sehemu za siri. Tumia kwa wastani ili kuzuia kuwashwa au kukauka sana kwa ngozi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS