Ijumaa, 2 Mei 2025

MTOMOKWA/MTOPETOPE

MTOMOKWA/MTOPETOPE

Mtomokwa/Mtopetope pori,Ni mmea unaozaa matunda yanayoitwa matomokwa ambayo yanakuwa na muonekano wa kijani au wekundu kwa nje ndani ikiwa na nyama nyeupe zenye kokwa nyeusi unaotumiwa sana katika dawa za asili za Kiafrika. Inakua katika sehemu nyingi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na inathaminiwa sana kwa umuhimu wake wa matibabu. Sehemu zinazotumika katika dawa asili ni Majani Gome (shina na gome la mizizi).

Faida za mtomokwa katika tiba asili:

1. Majani hutibu maambukizi ya ngozi uvimbe na maumivu ya viungo na majeraha.

2.Majani yake husaidia kupunguza homa (pamoja na inayohusiana na malaria).

3.Majani yake hutumika kwa kikohozi, pumu, na maumivu ya kifua.

4.Majani yake huondoa maumivu ya tumbo na kuhara.

5.Magome yake hutibu maambukizi ya bakteria na magonjwa ya zinaa.

6.Magome yake hutumika kwa maumivu ya meno na mwili.

7.Magome yake husaidia kuondoa sumu kupitia mkojo.

8. Mizizi hutumika kwa minyoo ya matumbo.

Jinsi ya kutumia:

1.Chemsha:Majani mabichi au yaliyokaushwa (kiganja) kwenye maji ya moto kwa dakika 10-15. Kunywa kikombe 1, mara 2-3 kwa siku.

2.Bandika:Majani mabichi yaliyosagwa bandika moja kwa moja kwenye majeraha au maeneo yaliyovimba.

3.Kuvuta pumzi ya mvuke: Chemsha majani na vuta mvuke kwa tatizo la kupumua.

4.Chemsha magome (10-20g) katika maji kwa dakika 15-20. Chuja na chukua kikombe nusu mara 2 kwa siku.

5.Dawa ya maumivu ya jino: Tafuna kipande kidogo cha gome la shina au maji ulorowekea magome yake kuosha kinywa au kuskutuwa.

6.Chemsha vipande vidogo vya mizizi iliyokatwa (5-10g) katika maji, chuja, na unywe kwa kiasi (1/4-1/2 kikombe, mara moja au mbili kwa siku).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS