MLANGAMIA
Mlangamia,Ni mti ambao shina lipo chini mti upo juu huwa na sifa mfano wa kambakamba au nywelenywele unapoota hauonyeshi kuwa unaelekea wapi ambao hutumika katika tamaduni mbalimbali.
Faida za Mlangamia katika tiba asilli:
1.Husaidia kupunguza uvimbe na kukuza uponyaji wa majeraha.
2.Husaidia tatizo la kwikwi yenye muendelezo.
3.Husaidia ngozi ya kichwa na kukuza ukuaji wa nywele.Inatumika kuimarisha nywele, kupunguza mba, na kuchochea ukuaji.
4.Husaidia kuondoa maumivu ya tumbo la hedhi/chango la wakina mama.
5.Husaidia kuondoa homa za msimu kwa kuchanganywa na miti mingine katika kujifukiza.
6.Husaidia kusafisha mfumo wa uzazi .
7.Huondoa maumivu ya tumbo kwa watoto na watu wazima pia.
8.Hutumiwa kusafisha ngozi.
9.Husaidia mtoto aliebemendwa kwa kunyweshwa na kuogea.
10.Huondoa homa za upepo na kuupa mwili nguvu kwa kujifukiza nyungungu.
Jinsi ya kutumia mlangamia katika tiba asili:
1.Kwa majeraha au kuvimba:kuchemshwa kwa maji na yakipoa osha moja kwa moja kwenye ngozi.Nakamba zake twanga na ubandike kwenye kidonda
2.Kwa kusafisha mirija ya uzazi:Chemsha mlangamia kwa maji na kunywa 1/4(Robo) kikombe cha chai.
3. Matibabu ya Nywele chemsha na kutumia kusuuza katika ngozi ya kichwa.
4.Kwa kwikwi:Chukua kamba za mlangamia na chembe za ubani 3.
5.Kwa mtoto aliebemendwa anyweshwe na kuogeshwa.Maji ya kuogeshwa wapekeche kamba hizo kwenye chombo wazazi wake na kumuogeshea mtoto huyo siku 21.
6.Kwa tumbo kamba zake ponda na maji uchuje unywe urojo wake kwa robo kikombe kutwa mara 2.
Zingatio:Hizo ni faida za mlangamia kwa uchache kuna faida nyingi zinapatika katika kamba zake na kiazi chake kwa ujumla kutokana na matumizi mbalimbali katika jamii tofauti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni