Alhamisi, 1 Mei 2025

KIVUMBASI/KIVUMBASHA

KIVUMBASI

Kivumbasi ni mmea wa dawa unaotumika sana katika tiba za asili nchini Tanzania na maeneo mengine ya Afrika Mashariki. Ingawa kuna mimea kadhaa inayojulikana kwa jina hili kulingana na eneo na kabila, moja ya mimea inayojulikana zaidi kama Kivumbasi ni aina ya mimea yenye harufu nzuri(ambayo ni pamoja na mimea ya mnanaa na majani ya chai).

Faida za Kivumbasi katika tiba asili:

1.Kivumbasi hutibu uzazi ulifungwa kiuchawi.

2.Hutibu tatio la kikohozi na mafua.

3.Kivumbasi hutuliza maumivu ya kichwa na mwili.

4.Kivumbasi na manyoya ya kuku na mbuzi ukimfusha mtu mwenye degedege anapona.

5.Kivumbasi ukinywa kwa wingi hutoa uchawi mwilini.

6.Maji ya kivumbasi huondoa uchovu na kuongeza nguvu.

7.Kivumbasi hutibu na tatizo la presha.

8.Husafisha nyumba na mambo ya kisihiri.

9.kivumbasi huondoa nuksi mwilini jifukize Na kunywa kwa siku 14.

10.Hutoa mafuta mwilini kwa kupunguza unene.

11.Hutibu magonjwa ya tumbo na kwa wasioona siku zao/hedhi.

12.Husaidia kwa mtoto mchanga asiyepata choo.

13.Kivumbasi kwa aliyekumbwa Na jini mbaya na athari zote alizosababishiwa na jini.

Jinsi ya kutumia kivumbasi katika tiba asili:

1.Anayeumwa tumbo anywe kwa nusu kikombe kwa mtu mzima na mtoto basi mpe kijiko kimoja cha maji ya kivumbasi.

2.Dekia maji ya majani ya kivumbasi pia choma kivumbasi kikavu ufukize moshi wake.

3.Maji ya kivumbasi kwa wingi nakuoga athari zilizompata kwa upepo mbaya zitaondoka.

4.Majani yake huchemshwa na mvuke wake kujifukiza .

5.Kivumbasi kikavu na unga wa sembe kichome pamoja kwa kusafisha nyumba.

6.Chemsha kivumbasi Na kunde mbichi Saba hutoa kifungo cha mwanamke aliyefanyiwa sihiri asipate mimba.

7.Manyoya ya mbuzi na ya kuku basi unamfukiza mtu aliyeanguka mtu mwenye degedege atapona.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS