Jumatatu, 24 Februari 2025

MPERA

Mpera ni mti wa matunda ya kitropiki yenye virutubishi vingi na hutumika sana matunda yake kama chakula na pamoja na mmea wake ikiwa ni matunda, majani na magome yake pia katika tiba asili.Hivyo kwa matumizi ya mmea huo hupatikana afueni katika maradhi mbalimbali. Faida za Mimea wa mpera katika tiba asili:

1.Husaidia kuimarisha mfumo wa kinga na kulinda dhidi ya maambukizo na magonjwa.

2.Nyuzinyuzi kwenye mapera husaidia usagaji chakula vizuri na kuzuia tatizo la kuvimbiwa na kujaa kwa gesi tumboni.

3.Mapera husaidia kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu, na kuifanya kuwafaa watu wenye kisukari.

4.Husaidia kupunguza shinikizo la damu, kupunguza viwango vya cholesterol, na kuboresha afya ya moyo kwa ujumla.

5.Mapera ni matunda bora kwa udhibiti wa uzito kutokana na uwepo wake wa nyuzinyuzi.

6.Husaidia kupunguza uvimbe mwilini na kupunguza hali kama vile ugonjwa wa yabisi.

7.Majani ya mpera husaidia uponyaji wa jeraha.

8.Majani na magome ya mpera hupunguza makali ya maumivu ya hedhi.

9.Majani ya mpera yamekuwa yakitumika kitamaduni kutibu magonjwa ya kupumua kama vile kikohozi, na mafua.

10.Majani ya mpera husaidia kudumisha usafi wa kinywa, kupunguza kuvimba kwa fizi, na kutibu vidonda vya mdomo.

11.Majani ya mpera husaidia katika kuzuia kuharisha au tumbo la kuharisha. Matumizi ya Mpera katika Tiba ya mitishamba:

1.Chai ya Majani ya Mpera:- Tia majani ya mpera kiasi katika sufuria nauwache yachemke na kuweza kutumia maji yake kwa manufaa mbalimbali katika mwili,1x3 kikombe kidogo cha chai .

2.Majani ya mpera twanga na majimaji kidogo na kubandikwa katika ngozi yenye majeraha au sehemu ulipojikata .

3.Magome ya Mpera:Chukua kiasi cha magome ya mpera na uweze kuchemsha katika sufuria na maji yakichemka uweze kutumia maji yake 2x3 ndani ya wiki moja,1x3 kikombe kidogo cha chai .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS