Jumatatu, 12 Agosti 2024

UVUMBA

UVUMBA

Uvumba,ni dawa yenye harufu nzuri na mafuta yake ambayo hutumiwa kama tiba asili, umetumiwa katika tamaduni mbalimbali kwa madhumuni ya kutibia kama dawa asili.Unapochomwa uvumba hutoa moshi wenye harufu nzuri ambayo huwa na athari za matibabu.

Faida za uvumba mkwa afya

1.Harufu ya uvumba husaidia kupunguza msongo wa mawazo na kukuza utulivu.

2.Uvumba huongeza umakini na uwazi wa kiakili.

3.Kuchoma uvumba kabla ya kulala huboresha usingizi.

4.Afya ya Kupumua:Una sifa za kuzuia uchochezi ambao unaweza kunufaisha afya ya upumuaji.

5.Uvumba husaidia kupunguza maumivu madogo na maumivu makali.

6.Uvumba husaidia kuficha harufu mbaya na kutengeneza mazingira mazuri.

7.Huondoa tatizo au kutibu tatizo la gesi tumboni.

8.Husaidia tatizo la bawasiri kwa kupunguza maumivu makali.

9.Husaidia na kuondoa tatizo la yabisi tumboni ambayo husababisha choo kigumu.

Jinsi ya kutumia uvumba katika tiba asili:

1.Uvumba hutumiwa kwa kusafisha eneo husika kitiba asili kwa kuchoma ili kupata moshi wake.

2.Uvumba huchanganywa na kivumbasi kuchemshwa pamoja kunawia maji yake kwa wenye matatizo ya bawasiri kutibia maumivu makali.

Tahadhari:Watu walio na hali ya kupumua kama vile pumu wanapaswa kutumia uvumba kwa uangalifu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS