MSHUBIRI/ALOE VERA
Mshubiri/Aloe vera, ambayo mara nyingi hujulikana kama aloe, mshubiri ni mmea wa kudumu na majani mazito yenye nyama ambayo yana dutu yenye jeli inayojulikana kwa sifa zake za dawa.Shubiri Imetumika kwa karne nyingi katika dawa za asili kwa faida mbali mbali za kiafya.Hulimwa sana kwa matumizi mbalimbali ya kiafya kama dawa asili kwa kutengeneza biadhaa mbalimbali.Halkadhalika pia kuna shubiri za vidonge ambazo ni shubiri duhani pia kuna shubiri aswed.
Faida za Aloe Vera/Mshubiri kiafya:
1.Jeli ya Aloe vera hutumika sana kwa ajili ya kulainisha, kutuliza na kuponya ngozi.
2.Aloe vera ina sifa ya kuzuia uchochezi, kupunguza uvimbe ndani na nje.
3.Uponyaji wa Vidonda:Jeli ya Aloe vera huharakisha uponyaji wa jeraha kwa kuchochea kuzaliwa upya kwa seli na kupunguza makovu.
4.Afya ya mmeng'enyo wa chakula:Ina athari ya kutuliza maumivu na hutumika kuondoa kuvimbiwa.
5.Husaidia kuongeza kinga ya mwili.
6.Afya ya Kinywa:Jeli ya Aloe vera hutumika katika utunzaji wa meno kwa sifa zake za antibacterial, kusaidia kusafisha kinywa.
7.Jeli ya alovera husaidia kukuza ukuaji wa nywele, na inapunguza m'ba inapopakwa juu.
8.Alovera husaidia kusafisha damu mwilini nakuondoa mchafuko wa damu unaweza kupelekwea maradhi kama ya mtoki.
9.Jeli ya Aloe vera huupaka juu ili kupunguza maumivu ya viungo na misuli, kuvimba na kukakamaa.
10.Husaidia kupunguza viwango vya cholesterol na kuboresha afya ya moyo inapotumiwa kwa mdomo.
11.Inasaidia kutibu kuchomwa na jua, sehemu iliyoungua kwa moto, majeraha na maumivu yakuumwa na wadudu.
Jinsi ya kutumia Aloe Vera/Mshubiri kama dawa ya mitishamba:
1.Jeli ya Aloe Vera:Jeli inayotolewa kwenye jani la ndani Hupakwa kwenye ngozi kwa majeraha ya kuungua na kusafisha ngozi kuifanya kuwa nyororo.
2.Juisi ya Aloe Vera/mshubiri hutumiwa kunywa kama kirutubisho cha lishe kwa afya ya mmeng'enyo wa chakula, usaidizi wa kinga mwilini, na siha kwa ujumla.
3.pia shubiri ya kidonge huyeyushwa au kufanywa zinto kwa kutia maji kidogo hutumiwa kwa kunywa na kuweza kusafisha damu kuondoa majeraha chunusi muwasho upele na harara .
-Tahadhari: Mjamzito au anayenyonyesha, au kutumia dawa.Shubiri ni dawa kali mjamzito asitumie inaweza kumsabibishia kuharibu ujauzito na kwa mama anaenyonyesha ikamsabibishia athari kwa mtoto pia kwa matumizi ya ndani kwa ujumla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni