Jumamosi, 27 Julai 2024

NUNGUNUNGU

NUNGUNUNGU

Nungunungu, Ni wanyama wanaojulikana kwa miiba yao au miiba mikali inayofunika miili yao ambayo huwa wakiitumia miba hiyo kama silaha pale wanapotaka kushambuliwa kwa kuirusha. Wanapatikana katika mikoa mbalimbali na duniani kote, ikiwa ni pamoja na Amerika, Afrika, na Asia.Nungunungu wamehusishwa na matumizi na sifa mbalimbali za kimatibabu.

Zifuatazo ni faida za nungunungu katika dawa asilia:

1.Aromatherapy:Ngozi yake yenye miba hutumika kwa kutibia wakina mama maziwa yalovimba na kuuma au kuskia maumivu makali kusababisha maziwa hayatoki wakati wa kunyonyesha.

2.Husaidia matatizo yakutookwa kwa damu za pua kwa kujifukiza miiba yake pia kwa kuchanganya na majani makavu ya mbaazi.

3.Miba yake hutumika kama sindano au zana za kuondoa vipande au meno ya sumu kwa kuumwa na nyoka.

4. Mafuta ya nungunungu husaidia kusafisha ngozi ikiwa kutibia ngozi kama harara na mikunjo .

5.Mafuta ya nungunungu Yalitumika kitamaduni kwa ajili ya kutibu majeraha na maumivu ya baridi yabisi.

Matumizi ya miba ya nungunungu:

i.Chukua miba ya nungunungu kwa wamama wanaokuwa maziwa kuvimba na kuleta maumivu makali kiasi hayatoki choma miba yake huku moshi ukikupiga katika kifua chako ndani ya siku 3-5.

ii.kwa matatizo ya kutokwa damu puani chukua majani ya mbaazi na miba ya nungunungu upashe moto usage nakuchoma pamoja ukivuta mvuke wake na unuse unga huo wneye mchanganyiko wa majani mabichi ya mbaazi na unga wa miba ya mbaazi nakutumia damu itakata.

iii.ikiwa mafuta yake utapaka katika ngozi na kupata matokeo mazuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS