Jumanne, 11 Februari 2025

MMEA WA USINIGUSE

MMEA WA USINIGUSE

Mmea wa usiniguse , unaojulikana kama mmea nyeti, ni mimea ambayo inapatikana katika maeneo ya tropiki duniani kote.Ni maarufu kwa uwezo wake wa kukunja majani yake yanapoguswa au kutikiswa. dawa za kiasili. Majani, mizizi na mbegu zake zote zinathaminiwa kwa sifa zake za dawa.

Faida za Kiafya za mmea wa usiniguse katika Tiba ya Asili

1.Husaidia kuponya majeraha kwa sababu ya sifa zake za kutuliza.

2.Husaidia kupungunguza uvimbe wa ngozi,uvimbe wa mwili na maumivu ya viungo.

3.Pia mmea husaidia kuzuia kuharisha au kuendesha.

4.Mbegu za mmea wa usiniguse husaidia kutibu minyoo ya matumbo.

5. Husaidia kuondoa mfadhaiko, wasiwasi, na kukosa usingizi.

6.Husaidia kutuliza maumivu kwa kutibu hali kama vile maumivu ya kichwa na maumivu ya meno.

7.Husaidia mfumo wa umeng'enyaji na kusaidia matatizo kama vile kuvimbiwa na kumeza chakula.

8.Husaidia kutibu majeraha ya moto, vipele, chunusi, na matatizo mbalimbali ya ngozi.

Jinsi ya Kutayarisha na kutumia mmea wa usiniguse katika tiba asili.

1. Chai ya Majani ya mmea wa usiniguse:- Vijiko 1-2 vya majani kavu ya Majani ya usiniguse - 1 kikombe cha maji ya moto,Husaidia na msongo wa mawazo, mmeng'enyo wa chakula, na maambukizo mepesi.

2. Bandika majani yake uloyaponda:- Ponda majani mabichi paka moja kwa moja kwa eneo lililoathiriwa.

3.Saga mbegu ya Mmea wa usiniguse:- Tumia vijiko 1-2 vya unga wa majani ya mmea wa usiniguse uliochanganywa na maji au juisi.

4.Kijiko 1 cha mizizi ya mmea wa usiniguse kwa vikombe 2 vya maji chemsha na chuja na unywe kikombe 1/4, mara mbili kwa siku.Huzuia kuhara.

Tahadhari na Mazingatio - Ujauzito na Kunyonyesha:Epuka kutumia kwani huenda isiwe salama katika vipindi hivi.Kuzidisha kipimo kunaweza kusababisha athari zisizohitajika. Pia kwa wenye mzio na dawa na hii wanaweza kuacha matumizi haraka isijekuwaletea athari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS