NGOGWE
Ngogwe, ni mmea unaozaa matunda ya kijani nayakiiva huwa na rangi ya njano yenye ladha ya uchungu ambayo umbo lake kama nyanya.Tunda hili hutumiwa katika mapishi kupikiwa katika mboga na mchuzi. asili yake Amerika Kusini. Ingawa ngogwe inajulikana sana kwa matumizi yake ya upishi, pia ina faida mbalimbali za afya na matumizi katika dawa za asili.
Faida za ngogwe katika tiba asili
1.Husaidia kulinda mwili na kupunguza hatari ya magonjwa ya muda mrefu.
2.Ina vitamini C ambayo husaidia kuongeza kinga na kupigana na maambukizo.
3.Ngogwe husaidia katika usagaji chakula, husaidia kuzuia kuvimbiwa, na kukuza utumbo wenye afya.
4.Hudhibiti uzito kwa kuwa na yasifa ya tunda lake kuwa na nyuzizi.
5.Husaidia afya ya moyo,potasiamu katika ngogwe husaidia kudhibiti shinikizo la damu, na hupunguza viwango vya cholesterol.
6.Hupunguza uvimbe katika mwili na kupunguza hali kama vile ugonjwa wa yabisi.
7.Afya ya Macho:Ngogwe ni chanzo kizuri cha vitamini A ambayo husaidia kuimarisha uono.
8.vitamini C katika ngogwe husaidia kukuza uzalishaji wa collagen ambayo husaidia ngozi kuwa katika hali nzuri.
9.Husaidia kurekebisha viwango vya sukari ya damu .
10.Kuondoa sumu mwilini ambayo husaidia kusafisha ini na figo.
11.Husaidia matatizo ya pumnzi kama vile pumu na bronchitis, kwa sababu ya sifa zake za kuzuia uchochezi na kuongeza kinga.
12.Huimarisha mifupa yenye nguvu na yenye afya.
13.Husaidia afya ya ubongo, kuboresha hisia, kumbukumbu, na kazi ya utambuzi.
Matumizi ya ngogwe katika Tiba ya mitishamba
1.Matunda:Kula ngogwe safi au saladi ni njia ya kawaida ya kufurahia manufaa yake ya afya .
2.Majani ya ngogwe na matunda yanaweza kutumika kutengeneza chai ambayo hutumiwa kama kinywaji kwa manufaa ya kiafya.
3.Majimaji ya ngogwe hutumika kupaka kwenye ngozi juu ili kuboresha afya ya ngozi, kupunguza uvimbe, na kutibu majeraha madogo au hali ya ngozi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni