Jumamosi, 16 Novemba 2024

MNANAA PORI

MNANAA PORI

Mnanaa pori ni mnanaa mseto inatambulika sana kwa sifa zake za matibabu. Ni mojawapo ya mitishamba inayotumika sana katika dawa za asili na za kisasa kutokana na harufu yake ya kuburudisha, ladha na manufaa mbalimbali ya kiafya.

Faida za Kiafya za Tiba Asilia ya mnanaa pori

1.Mnanaa pori husaidia usagaji chakula,kuondoa kuvimbiwa, na gesi.

2.Mnanaa pori au kuvuta pumzi ya mafuta yake huondoa kichefuchefu .

3.Mnanaa pori husaidia kusafisha njia ya upumuaji na kurahisisha kupumua kutibu mafua, hutuliza kikohozi na msongamano wa kambaku.

4..Hutibu shida za utumbo, maumivu ya kichwa na mafadhaiko.

5.Mnanaa pori ni antibacterial ambayo husaidia kuua bakteria mdomoni,ambayo husaidia usafi wa kinywa kupunguza harufu mbaya ya mdomo.

6.Harufu ya mnanaa pori huboresha kumbukumbu, Kuvuta pumzi ya mafuta yake au kunywa chai yake husaidia kuboresha uwezo wa kiakili.

7.Mafuta ya mnanaa pori huzuia maambukizo ya ngozi, kupunguza kuwashwa, na kutibu magonjwa kama vile chunusi na ukurutu.

8.Mnanaa pori husaidia kupunguza wasiwasi, na uchovu wa akili.

9.Mnanaa pori husaidia mfumo wa kinga katika kupambana na maambukizi.

10.Mnanaa pori husaidia kupunguza maumivu ya hedhi.

11.Mnanaa pori husaidia kupunguza uzito kwa kukandamiza hamu ya kula na kuboresha mfumo wa umeng'enya

12.Mnanaa pori ni antimicrobial, na kutibu maambukizo, haswa katika mfumo wa usagaji chakula na upumuaji.

13.kupunguza dalili za mizio kama vile msongamano na kuwasha.

14.Mnanaa pori hulegeza misuli laini, na kuifanya iwe na ufanisi katika kutibu hali zinazohusisha na mkazo wa misuli

15.Hupunguza hisia za uchovu na kuongeza utendaji wa kimwili.

16.Hutibu shida za utumbo, maumivu ya kichwa na mafadhaiko.

17.Mnanaa pori hutumiwa katika aromatherapy maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, na masuala ya kupumua.

Jinsi ya kutumia mnanaa pori

1.Kuvuta pumzi ya mafuta ya mnanaa pori kuvuta pumzi ya mvuke kunaweza kusaidia kuondoa msongamano wa pua, kuboresha umakini, na kupunguza maumivu ya kichwa.

2.Mafuta ya mnanaa pori hupakwa kwenye ngozi ili kupunguza maumivu, kupunguza kuwashwa, na kutibu chunusi.

3.Mnanaa pori husafisha kinywa na meno pia huburudisha pumzi.

4.Majani ya mnanaa pori au mafuta huongezwa katika maji ya kuoga kwa ajili ya kupunguza msongo wa mawazo ambao hutuliza maumivu ya misuli.

5.Chai ya mnanaa pori au mafuta hutumika kwa maumivu ya kichwa, homa, na kuwashwa ngozi.

6.Majani safi au yaliyokaushwa ya mnanaa pori hutumiwa katika kupikia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS