MURU
Muru,Ni dawa iliyokaushwa na kufanywa kuwa katika vipande pande na ikiwa na rangi nyeusi kwa kawaida hujulikana kama tiba ambayo ni mara nyingi hutumika kusaidia watoto kwa matatizo mbalimbali.Dawa hii hutumiwa katika tiba ya asili , haswa katika tamaduni za India na Kusini-mashariki mwa Asia, kutokana na faida zake za kutibia maradhi mbalimbali.
Faida za Kiafya za Dawa ya Asili ya Muru.
1.Husaidia mfumo wa umeng'enyaji chakula, kupunguza asidi, na kuondoa dalili za kutokusaga chakula na kuvimbiwa.
2.Husaidia kudhibiti viwango vya sukari ya damu na kuwa yenye manufaa kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari.
3.Husaidia kutibu tatizo la tonsili kwa rika lote.
4.Husaidia kupunguza uvimbe wa tumbo kwa kuumwa kwa kitomvu au tovu kwa watoto wachanga.
5.Hupakwa kwenye ngozi husafisha ngozi na kuponya majeraha au maradhi ya ngozi na kuifanya kuwa soft.
6. Husaidia katika udhibiti wa uzito na kupunguza mkusanyiko wa mafuta.
7.Husaidia watoto kwa wale walobonyea au kuingia ndani kwa utosi.
Matumizi ya Muru katika tiba asili
1.Huyayushwa katika maji na kunywewa kama dawa asili kwa kupewa mtoto mwenye kusokotwa na tumbo kijiko kidogo kile kabisa 1x2.Kwa mtu mkubwa robo kikombe cha kahawa.
2.Hurowekwa na kufanywa nzito kiasi kupakwa katika ngozi au utosi uloingia ndani kwa mtoto.
3.Pia unaweza kutumia poda yake kuchanganya na maji kuifanya nzito na kupaka usoni kama maski.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni