Jumanne, 19 Novemba 2024

MTURA

MTURA

Mtura, Ni miti yenye shina na mizizi meupe midogo ambayo majani yake yakijani kibichi yenye vinywelenywele na shina lake ambalo lina miba miba mikali inayotoa mauwa ya zambarau na njano ambayo hutambulika kwa faida za kuwa dawa ya asili ikiwa shina, majani yake na matunda yake,Matunda hayo yanayotambulika kwa jina la tura/ndulele/tunguja/nyanya chungu.Ambayo inapatikana Afrika mashariki,afrika magharibi na nchi nyinginezo.

Faida za mtura katika tiba ya asili

1.Majani ya mtura hutumika kutibu matatizo ya usagaji chakula, hali ya upumuaji na kusaidia afya kwa ujumla.

2.Hupakwa kwenye ngozi kutibu vipele, majeraha na ukurutu.

3.Dawa za kikohozi ambayo husaidia kupunguza kikohozi na msongamano wa kupumua.

4.Hutumika kutuliza kuhara damu na masuala mengine ya usagaji chakula.

5.Majani ya mtura hutumiwa kwenye vidonda ili kukuza uponyaji na kuzuia maambukizi.

6.Majani ya mtura kutibu majeraha madogo na maambukizo kwa sababu ya sifa zao za antimicrobial.

7.Majani ya mtura husaidia kuzuia/kukata damu inayotoka kwa kasi.

8.Mizizi ya mtura husaidia kutibu matatizo ya tumbo kama kuumwa tumbo la ngiri au chango kwa wakina mama.

9.Mizizi ya mtura hutibu kinywa kutokana na maumivu ya meno na finzi.

10.Pia mauwa ya mtura ni dawa ya kiasili inayotumika kusafisha.

11.Tura zenyewe hutumika katika tiba asili kama dawa ya kuondoa jicho na hasadi na mengine mengi.

12.Tura pia vilevile hutumika katika kidonda kutibu kwa kujipaka maji yake.

13.Majani ya mtura hutumika kupunguza homa mwili.

14.Majani ya mtura hutumika kama dawa ya kutibu malaria.

Matumizi ya mtura katika tiba asili

1.Mizizi yake unachemsha na kunywa maji yake kama dawa ya tumbo ,ngiri n.k.

2.Majani yake unatwanga na kubandika sehemu ya jeraha ambalo linatoka damu.

3.Tura zenyewe zinatumika unapasua na kupaka sehemu husika.

4.Mauwa yake unayakausha juani nakutumia kuyachoma kusafisha dawa ya tiba asili.

5.Majimaji ya tura hutumiwa kama dawa ya sikio linaloleta maumivu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS