Jumanne, 20 Agosti 2024

MPAPAI

MPAPAI

Mpapai, unaojulikana kisayansi kama Carica papaya, Ni mti wa matunda wa kitropiki wenye asili ya Amerika ya Kati na Kusini mwa Mexico.Kuna faida mbalimbali zinazotumika katika mpapai ikiwepo tunda lenyewe, mizizi na mbegu:

Zifuatazo ni faida za Kiafya za Mizizi ya mpapai,majani ya mpapai na mbegu zake:

1.Husaidia kupunguza matatizo ya mmeng'enyo wa chakula kama vile kuvimbiwa na kukosa kusaga chakula.

2.Mizizi ya mpapai kwa kitamaduni hutumika kutibu minyoo ya utumbo na vimelea.

3.Kuzuia Uvimbe:Mizizi ya mpapai ina sifa ya kuzuia uvimbe, hivyo kupunguza uvimbe katika hali kama vile ugonjwa wa yabisi.

4.Mizizi ya mpapai ina vitamini ambayo inasaidia kazi ya kinga ya mwili na afya kwa ujumla.

5.Mizizi ya mpapai inasaidia afya ya ini na kuondoa sumu mwilini.

6.Mbegu za papai hutumika katika kutunza ngozi, kusaidia kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kukuza ngozi nyororo.

7.Majani ya mpapai yaliyosagwa au mabichi yaliyopondwa yanaweza kupakwa kwenye majeraha au muwasho wa ngozi kwa ajili ya uponyaji na athari za kutuliza.

8.Utomvu wake papai unasaidia kutibu mipasuko ya yabisi kama vile mipasuko ya miguu.

9.Majani ya mpapai yanasaidia kutibu homa za ndani kwa ndani kama vile homa ya dengu.

10.Mizizi ya mpapai dume hutumika kusafisha mirija ya uzazi kwa wakina mama.

11.Huondoa tatizo la yabisi tumboni nakusababisha kulainisha choo hivyo kuweza kusaidia kwa wale wenye matatizo hayo na bawasiri.

Jinsi ya kutumia mpapai kama dawa ya mitishamba:

1.Mizizi ya mpapai inachemshwa na kunywiwa maji yake kwa afya ya usagaji chakula na msaada wa kinga. Inaweza pia kutumika kwa hali ya ngozi.

2.Unga wa Mbegu za Papai au mbegu mbichi husaidia mfumo wa umeng'enyaji na tatizo la yabisi.

3.Majani ya mpapai yaliyosagwa yanaweza kupaka kwenye majeraha au muwasho wa ngozi kwa ajili ya uponyaji na athari za kutuliza.

4.Tumia papai na tumba chache kula pamoja mara kwa mara.

5.Osha majani ya mpapai vizuri na uweze kutumia maji yake kutwa mara mbili.

-Hitimisho:Mpapai ni mti uliokuwa na faida ya kuondoa tatizo la yabisi hivyo wenye matatizo ya bawasiri wanapaswa kutumia mara kwa mara kwa sababu yakuepukana na choo kigumu, ambacho kitakachoweza kusababisha athari za ugonjwa wa bawasiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Uwa la jerusalem

UA LA JERUSALEM Ni mmea ambayo midogodogo kwa kawaida huwa hutoa mauwa ya pinki, meupe na zambarau. Zifuatazo ni faida za mti wa ...

POSTS